Baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kupokea mashine za kuchomelea (welding) kutoka Ofisi ya Rais ya Tamisemi kwa ajili ya kuwapatia kikundi cha Vijana Cha Mtwara Social Workers kilichopo Kata ya Likombe, Naibu meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Mhe. Edward Kapwapwa Novemba 1,2022 amekabidhi msaada huo kwa kikundi hiko wa kwa ajili ya kufanyia kazi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hizo Mhe. Kapwapwa ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwaunga mkono vijana katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa kutumia teknolojia za kisasa na amewataka vijana liopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuacha kukaa vijiweni badala yake wajitoe kufanya kazi.
Kwa upande wake Katibu wa Kikundi Cha Mtwara Social workwers Issa Utohi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia mashine hizo bila malipo yoyote na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia kwa muda mrefu.
Aidha vijana hao wameushukuru Uongozi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwasimamia vizuri na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.