NAIBU WAZIRI AIPONGEZA MANISPAA KWA KUTOA SHS.MILIONI 355 KWENYE MFUKO WA WDF
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Anastanzia Wambura ameipongeza halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani kwa kutoa fedha kiasi Tsh. 355,000,000/= kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake na Vijana.
Amesema kuwa halmashauri nyingi zinashindwa kutenga asilimia 10 ya bajeti yake kwa ajili ya kutunisha mfuko wa wananwake na vijana ili kuweza kusaidia makundi hayo.
Pongezi hizo zimetolewa kwenye kikao cha baraza la Madiwani lililofanyika Julai 26 katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa wakati wa kuipitia na kuijadili taarifa ya Miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyotekelezwa kwenye bajeti ya 2016/2017 kupitia Mapato ya ndani.
Mhe Wambura alisema kuwa kipindi cha nyuma wamekuwa wakizipigia kelele halmashauri kila wanapohudhuria vikao kwa sababu walikuwa wanatoa fedha chache kwenye mfuko huo kitu ambacho kilikuwa kinakwenda kinyume na maagizo yanatotolewa na viongozi wa juu.
“Baadhi yenu ni mashahidi hapo nyuma tulikuwa tunafika hapa kwenye vikao ukiangalia fedha zilizotolewa kwenye mfuko wa wanawake na Vijana ni milioni 20, Leo hii tunaona fedha zilizotolewa milioni 355 ni hatua kubwa kwa kweli mnastahili pongezi”alisema Wambura
Aidha Wambura aliipongeza Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuandaa tarifa nzuri ambayo inaonesha uhalisia wa nini kimefanyika mwaka mzima na hivyo kuweka uwazi na kuondoa maswali na mashaka kwa wajumbe.
Pia amewataka watendaji na Madiwani kushikamana na kufanya kazi kwa kwa umoja, ili kuleta Maendeleo ya Wana Mtwara
Manispaa Mtwara-Mikindani kwa mwaka fedha ulioishia 2016/2017 imekusanya kiasi cha Shs. Bilioni 3,782,747,372.72 Kutoka mapato ya ndani na kupeleka kwenye mfuko wa wanawake na vijana shs.355 ambayo ni sawa na asilimia 93.85Aidha vikundi 62 vya wanawake na vikundi 22 vya Vijana vimepata mikopo na kufanya jumla ya vikudi 84 vilivyokopeshwa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.