Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mtwara Mjini, Mhe. Salum Naida, amewapongeza madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa juhudi zao kubwa katika kuwahudumia wananchi, ikiwemo usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza leo, tarehe 8 Mei 2025, katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za Halmashauri kwa robo ya tatu ya mwaka 2024/2025 uliofanyika katika ukumbi wa Boma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, amesema madiwani hao ni wenyeviti wa kusimamia maendeleo katika kata zao, kwani miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa katika manispaa hiyo inatekelezwa ndani ya kata zao.
Amesema jukumu la baraza hilo ni kuleta maendeleo, kusikiliza hoja za wananchi, kuzifanyia kazi na kutoa mrejesho ambao utachangia katika ustawi wa jamii ya Mtwara Mjini.
“Na kazi hiyo mnaifanya ninyi madiwani kwa kushirikiana na wataalamu. Hivyo, nawatakia mafanikio mema; tangu baraza hili lilipoanza hadi sasa, maendeleo yanaonekana na wananchi wanayajua,” alisema Nahida.
Aliongeza kuwa, ikiwa kikao kimoja pekee kimebaki kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo, ni vyema viongozi hao wakaacha taswira nzuri kwa jamii, hususan kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.