Baada ya kupokea madarasa ishirini na moja ya Sekondari viti Pamoja na meza 840 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko Desemba 21,2022, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameipongeza Manispaa hiyo kwa kukamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati na katika viwango vilivyokubalika.
“Tumekuja kufanya ukaguzi na kupokea madarasa, kwa kweli madarasa yanapendeza na nimeridhia kuyapokea ni mazuri sana, ujenzi umeenda kwa viwango vilivyowekwa na madawati yapo madarasani, niipongeze ofisi ya Mkurugenzi kwa usimamaizi mzuri” amesema Mhe.Kyobya
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mhe. Salumu Naida amempongeza Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Mkuu wa Wilaya, Viongozi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa usimamizi mzuri wa madarasa hayo na kwamba Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara kimeridhika na usimamaizi huo.
‘Nimeona kazi, kazi ambayo inaridhisha sisi kama chama cha Mapinduzi tunasema kuwa hii kazi imeenda vizuri na tunaomba maeneo yote kazi zifanyike vizuri kama zilivyofanyika hapa ili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Januari waripoti shuleni.
Nae Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe.Hassan Mtenga ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi pamoja na walimu kwa kazi nzuri yenye kuridhisha.Aidha amekipongeza Chama kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa kushauri wa masuala mbalimbali
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa Manispaa kwa sasa haina upungufu wa madarasa baada ya kupokea fedha shilingi milioni mia nne ishirini za ujenzi wa Madarasa ishirini na moja ya Sekondari mwezi Septemba mwaka huu .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.