Katika kuhakikisha kuwa vijana wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wanashiriki michezo ili kujenga afya zao Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile ameandaa ligi ya mpira wa miguu ijulikanayo (Ndile Meya Cup) ambayo itazinduliwa rasmi Mei 30 mwaka huu ikihusisha timu kumi na nane zilizopo kwenye Kata zote za Manispaa.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Mei 19, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Shadida amesema kuwa ameanzisha ligi hiyo kwa lengo la kuhamasisha michezo ili kuibua vipaji na kuwatafutia njia vijana hao kuelekea timu kubwa.
Amesema kuwa Pamoja na kuibua vipaji ligi hiyo pia itaimarisha upendo na mshikamano kwa vijana Pamoja na kuwapunguzia muda wa kukaa vijiweni ili kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya,ambayo kwa kiasi kikubwa yanaathiri ukuaji wa uchumi wa nchi .
Ameendelea kufafanua kuwa katika mashindao hayo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi ikiwemo fedha taslimu pamoja na ufadhili kwa washiriki wakiwemo wachezaji na waamuzi wa mpira.
Kwa upande wake Katibu wa kamati ya Maandalizi Kasimu Ngumbi amesema kuwa katika hatua za awali ligi hiyo itachezwa katika viwanja vitatu vilivypo Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani vikiwemo viwanja vya TARI Naliendele, Nangwanda Sijaona Pamoja na viwanja vya Titanic Vilivyopo Mikindani.
Mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ya Ndile Meya Cup yatazinduliwa na Mkuu wa Mkoa katika Viwanja vya mpira wa miguu vilivyopo TARI-Naliendele na yatamalizika Julai 17 mwaka huu yakiwa na kauli mbiu inayosema “ Manispaa yetu, Michezo yetu, Ajira yetu”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.