Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani, Mhe. Shadida Ndile akishirikiana na Wanawake toka Bodi ya korosho Mtwara, wametoa msaada wa vifaa vya usafi na vinywaji baridi katika Zahanati ya Rwelu na kituo cha afya Mikindani ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Akitoa neno baada ya kukabidhi msaada huo Meya Ndile alisema lengo ni kuhakikisha hali ya usafi katika vituo vya afya Pamoja na kuboresha afya za wakazi wa maeneo husika kwani afya ndio mtaji mkubwa wa mwanadamu yeyote.
Kwa upande wao, Mkuu wa Idara wa Maendeleo ya Jamii BI. Mwanamtama pole waliwaomba wahusika kuvitunza vifaa hivyo kwa kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Vifaa vya usafi vilivyotolewa ni Pamoja na Mifagio, sabuni za maji, sabuni za unga, ndoo maalum za kudekia, Makwanja slashers, Mashuka na vinywaji baridi.
Siku ya wanawake duniani itaadhimishwa siku ya kesho tarehe 08 Machi, 2025 ikiwa ni kauli mbiu, wanawake na wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na uwezeshaji.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.