Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen Marco Gaguti amesema kuwa ana tamani sana kuiona Manispaa yetu ya Manispaa yetu ya Mtwara-Mikindni inakua kiuchumi.
Ili kufanikisaha hilo Mkuu wa Mkoa amemuomba Mstahiki Meya, Baraza la Madiwani na wataalamu kuwa wabunifu katika kuibua vyanzo vya mapato na kuvisimamia.
Mhe.Gaguti ameongea hayo Juni 14,2021 kwenye Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Boma Mkoa.
Amesema kuwa hayo yote yatafanikiwa kama wataalam ,viongozi na wananchi watashirikian ili uchumi wetu uweze kukua kwa haraka.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi.Shadida Ndile amememshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuonesha ari ya dhati ya kutaka kuinua uchumi wa wana mtwara.
Aidha ameahidi kuendelea kuwasisitiza viongozi katika kudumisha mshikamano na kuwa wabunifu katika kuibua vyavzo vipya vya mapato na kuvisimamia.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.