Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya amesema kuwa anaridhishwa na namna Manispaa ya Mtwara-Mikindani inavyotekeleza miradi ya Maendeleo katika maeneo yake na amewapongeza Waheshimiwa Madiwani na Mkurugenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi yenye viwango vikubwa sana.
Mhe.Mwaipaya ameyasema hayo Leo Mei 8,2025 kwenye mkutano wa baraza la Madiwani wa kupitia taarifa za halmashauri robo ya tatu 2024/2025 uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara (Boma)
Kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, Mhe.Mwaipaya amewasisitiza Madiwani kwenda kuwahamasisha wananchi wao kujitokeza kwenye zoezi la Uboreshaji wa taarifa za mpiga kura awamu ya pili linalotarajia kuanzia tarehe 16-22.05.2025.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.