Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ambae sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dustan Kyobya ameahidi kuwa balozi wa kuisemea vizuri Mtwara ili wadau wa maendeleo waweze kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana Mtwara na kuzichangamkia.
Ameyasema hayo leo februari 9,2023 kwenye makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Hanafi Msabaha ambae sasa ni Mkuu wa Wilaya Mtwara.
Licha ya ahadi hiyo Mhe. Kyobya amewaasa wananchi na wadau wa Mtwara kuendelea kutumia fursa zilizopo Mtwara ili kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe. Kyobya amewashukuru wanamtwara wote kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi chote alichokuwa anahudumu Wilayani hap ana kuwataka kuendelea kumpa ushirikiano Mkuu wa Wilaya ya Mtwara wa sasa ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.