Kufuatia kuwepo kwa wahanga walioathirika na mvua zilizonyesha kwa siku tano katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya amepokea chakula na vifaa mbalimbali kutoka benki ya NMB na Hotel ya Tiffany ikiwa sehemu ya msaada kwa jamii hiyo Leo Februari 11,2025.
Mhe. Mwaipaya amewashukuru wadau hao kwa namna walivyoguswa na kuamua kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wananchi waliopatwa na majanga hayo wanapata Faraja na mahitaji ya msingi yatakayowasaidia katika kipindi cha mpito.
Aidha Mhe.Mkuu wa Wilaya amewahakikishia wadau hao kuwa vitu vilivyotolewa vitawafikia walengwa wote na ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwasaidia wananchi waliopata athari ya mvua
Wadau hao wamekabidhi viroba vya unga, mchele, sukari, ndoo za mafuta, taulo za kike chumvi, sabuni za unga pamoja na vitu vingine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.