Wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kuchangia ujenzi wa uzio katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Chuno ambapo Leo Mei 17,2025 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeunga mkono juhudi za maendeleo za wananchi wa Kata hiyo kwa kuchangia matofali 500 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi tofali izo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi, Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Vivian Swai (aliyevaa koti la rangi ya maziwa) amesema kuwa , ofisi imetambua kazi kubwa iliyofanywa na wananchi katika kukuza sekta ya elimu hivyo amewapongeza wananchi hao kwa kujitolea kujenga uzio kwani utaimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi.
Aidha ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada za maendeleo za wazazi shuleni hapo kwa kuendelea kuchangia ujenzi wa uzio ili wanafunzi wasome vizuri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi shuleni hapo Bwana. Selemani Kadeghe ametoa shukrani zake za dhati kwa Ofisi hiyo kwa kuchangia maendeleo shuleni hapo na amewaomba waendelee kuchangia kwa kuwa ujenzi bado unaendelea huku akiwaomba wadau wengine Kwenda kuwaunga mkono ili waweze kumaliza ujenzi huo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Zahra Ramadhani ametoa shukrani kwa wadau hao kwa kuwezesha ujezi wa uzio kwani itawasaidi kusoma katika mazingira salama ambayo yatasaidia kuongeza ufaulu shuleni hapo na wameahidi kutowaangusha wadau wote waliochangia ujenzi huo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.