Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Ahmed Abbas Ahmed ametembelea mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Likombe na kuwapongeza wataalamu waliosimamia mradi huo pamoja na mafundi waliojenga na amezitaka Kamati zote zinazohusika na ujenzi huo kutekeleza wajibu wake Katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa viwango vinavyokubalika.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Ahmed Abbas Ahmed amewataka walengwa waliopo kwenye Mpango wa kunusuru Kaya maskini Mtaa wa Magomeni Kagera kuzitumia vizuri fedha wanazopewa kwa kufanya mambo ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba Pamoja na kusomesha Watoto wao
“Nimefarijka kuona usimamizi mzuri unaofanywa na wataalamu katika mradi huu Rai yangu kwa wananchi ni kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa Serikli ili mradi uweze kukamilika kwa wakati”
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akipokea taarifa ya Mradi wa Upimaji, upangaji na umilikishaji wa Viwanja Mjimwema (SAMIA CITY PROJECT) kutoka kwa Mratibu wa Mradi huo bwana Rugembe Maiga.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewasiistiza wataalamu wa Mipangomiji kusimamia na Mradi kuhakikisha Mji huo unapangwa vizuri kulingana na mpango uliopo na amewataka wananchi waliopata viwanja kukamilisha malipo kwa wakati ili Manispaa iweze kurejesha mkopo wa Bil. 1. Kwa Serikali..
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.