Kutokana na taarifa ya Mdhibiti Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) iliyosomwa juni 4 mwak huu na kuonesha kuwa katika mwaka wa fedha 2019/2020 Manispaa ya Mtwara- Mikindani tumepata hati safi 9 Unqualified Opinion), Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen Marco Gaguti ametupongeza kwa kupata hati hiyo.
Pamoja na pongezi hizo Mkuu wa Mkoa ametusisitiza kuweka Makzo kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani ili tuweze kufikia asilimia 100 au zaidi.
Ameendelea kusisistiza kila Mmoja wetu kuhakikisha anasimamaia vizuri matumizi ya fedha za umma iliziweze kutelekeza mipango yote iliyopangwa ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande walke Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtawra-Mikinfdani Col.Emauel Mwaigobeko amesema kuwa katika ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha wa 2019/2020 Manispaa ilikuwa na hoja ishirini kati ya hizo hoja kumi na tatu zimefungwa na hoja saba zipo kwenye utekelezaji.
Manispaa ya Mtwara –Mikindani tumekuwa tukifanya vizuri kwenye usimamizi wa matumizi mazuri ya fedha na kupelekea kupata hati safi kwa mara ya tano mfulilizo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.