Katika kuhakikisha kuwa Mkoa wa Mtwara unafanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa ya Shule za Sekondari na Msingi ikiwemo na ufutaji wa daraja sifuri , Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.jen.Marco Gaguti ameahidi kutoa shilingi milioni tano kwa shule ambayo itafuta daraja sifuri katika Mitihani ya taifa itakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Amesema kuwa lengo la kutoa fedha hiyo ni kujenga hamasa ya kazi na kutoa motisha kwa wale wote ambao watahusika wakiwemo walimu, watendaji wa Kata, Mitaa Vijiji na vitongoji.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo Februari 23,2022 katika kikao cha kufuatilia mkakati na utekelezaji wa mpango kazi wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Kawaida TTC.
Amesema kuwa ili kuweza kufikia malengo ya kuongeza ufaulu na kuondoa daraja sifuri ni lazima walimu kuwa na uwekezaji binafsi kwa kujiwekea malengo madogo madogo ili kutoa mchango kwenye Maisha ya mtanzania.
Pamoja na walimu kujiongeza Mhe. Gga8ti pia amewataka kuweka mipango mizuri ya kuhakikisha Watoto wote shuleni wanapata chakula pamoja na kuboresha mazingira ya shule ili mtoto abaki shuleni wakati wote na kufuatailia masomo.
Ili dhamira ya kuongeza ufaulu na kuondoa daraja sifuri iweze kukamilika , Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Ofisi yake itachapisha mitihani ya majaribio kwa madarasa ya mitihani kupitia taarifa ya elimu ya mwezi ya kila wilaya.
Kikao kazi cha kupitia mkakati wa utekelezaji wa mpango kazi wa Elimu umehusisha Wakuu wa Idara na Vitengo , Watendaji wa Kata na Mitaa ,walimu wakuu na wakuu wa shule Pamoja na waratibu Elimu Kata wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.RC Gaguti Kutoa Mil.5 Kwa Shule itakayofuta Daraja Skifuri
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.