Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Patrick Sawala amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani na kufurahishwa na jinsi Manispaa hiyo ilivyotumia Shilingi milioni 189,554,000 za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la kusubiria wagonjwa wa nje Mtawanya (143,459,000), Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Msikitini (33, 400,000) pamoja na ujenzi wa kisima cha maji Mtaa wa Mwera-Chikongola (12,695,000) .
“Mmefanya kitu chema kutoa mapato ya ndani na kusogeza huduma karibu na wananchi, Hongereni sana, miradi ni mizuri, tumeona kazi zilizofanywa kwa fedha za mapato ya ndani ya Manispaa amabzo zimewagusa walipa kodi wenyewe,”amesema RC Sawala
Aidha Mkuu wa Mkoa amefurahishwa na mradi wa ujenzi wa kisima cha maji katika Mtaa wa Mwera uliopo kata ya Chikongola kwa kuwa mradi huo unaenda kuwanufaisha wananchi wa Mtaa huo na maeneo ya jirani kwa kupata kupata maji safi na salama.
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa vijana wa uzalishaji wa tofali kata ya Ufukoni, Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Tandika Pamoja na Mradi wa ufunguzi wa Kituo cha Redio Cha HFM.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Leo Mei 7,2025 Mhe. Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara pamoja na watumishi kutoka katika sekta mbalimbali kama vile, TARURA, RUWASA, MTUWASA na TANROAD.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2025 Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani. All rights reserved.