Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenani Sawala amewaongoza mamia ya wakazi wa Mtwara katika zoezi la kujiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika nchini kote tarehe 27 Novemba, 2024.
Zoezi hilo ambao Kitaifa limezinduliwa leo tarehe 11, Oktoba, 2024 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, @samia_suluhu_hassan litaendelea mpaka tarehe 20 Oktoba,2024.
Kanali Sawala alitumia fursa hiyo kuongea na halaiki ilijiyojitokeza katika mtaa wa Shangani East ambapo alitoa wito kwa wananchi wote waliokidhi vigezo kujitokeza kutumia haki yao hiyo ya kujiandikisha ili waweze kupiga kura.
"Niwapongeza waandaazi wote wa mchakato huu lakini sifa zote ziende kwa Mhe. Raisi Samia Suluhu Hassan Kwa kutupatia fursa hiyo wananchi wote tukiwemo wanaMtwara ya kutimiza demokrasia yetu," alisema.
Aidha alipongeza Vijana kwa muitikio woa mkubwa kujitokeza katika zoezi hilo na aliwataka wanahabari kuendelea kutoa hamasa zaidi ya watu kujiandikisha.
#serikalizamitaasautiyawananchijitokezekushirikiuchaguzi
@mtwarars_habari
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.