Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Patrick Sawala ameitaka Menejimenti ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha inasimamia vyanzo vya mapato vilivyopo na kubuni vyanzo vipya pamoja na kusimamaia vizuri matumizi ya mashine za ukusanyaji wa mapato (POS) ili halmashauri iweze kutekeleza miradi ya maendeleo na wananchi wapatiwe huduma zinazostahiki.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo April 25,2024 kwenye kikao kazi na watumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kilichofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi ambapo kikao hicho kimelenga kujitambulisha tangu ateuliwe kuwa Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa anatarajia kuona huduma bora zinaendelea kutolewa kwa wananchi huku akiwasisitiza watumishi kutenga muda wa kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yao na kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia lugha nzuri na ya upole.
Ameendelea kusema kuwa anatamani kuiona Mtwara inafanya vizuri kwenye kila kitu hivyo ametaka kila mtumishi kutimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa uadilifu, kuondoa urasimu mahala pa kazi pamoja na kuwatendea haki watumishi waliochini yao.
Aidha amewasisitiza watumishi hao kuifanya ajenda ya usafi kuwa ya kudumu kwenye maeneo yao ili kuhakikisha Mji wa Mtwara unakuwa safi muda wote kama ilivyo miji mingine na amewataka wataalamu kujikita kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Moa huyo ameipongeza Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kufaulisha vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka uliopita na kupatiwa cheti hapongezi kutoka kwa Wazri wa TAMISEMI Mhe. Mohamedi Mchengerwa .
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Mwanahamisi Munkunda maesema kuwa atahakikisha naisimami halamshauri katika ukusnayaji wa mapato ili kuhakikisha Mkurugenzi analipa madeni ya watumishi na kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya kazi ndani ya Manispaa.
Kikao kazi hicho kiliwahusisha Wakuu wa Idara na Vitengo , Wakuu wa shule na walimu wakuu, Maafisa Elimu Kata, Watendaji wa Kata na Mitaa pamoja watumishi wa kada mbalimbali wanaofanya kazi katika ofisi za makao makuu ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.