Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL.Patrick Sawala ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kwa ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo ambayo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Amesema kuwa hana mashaka na Utendaji kazi waManispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwa wamekuwa wakifanya vizuri kwenye utekelezaji wa miradi akitolea mfano wa miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu iliyopelekea Manispaa kushika nafasi ya kwanza kimkoa, pamoja na kwenye sekta ya elimu na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ambapo Manispaa imekuwa ya pili kati ya Manispaa 20 zilizopo Tanzania bara na kutunukiwa tuzo.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo Leo Desemba 23,2024 alipokuwa Kwenye ziara ya Ukaguzi wa miradi ya Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Magomeni na matundu ya vyoo sita (58,200,000) na Ujenzi wa Majengo matano Hospitali ya Wilaya Mjimwema(1,000,000,000).
Kwa upande wa mradi wa madarasa na matundu ya vyoo COL.Sawala amesema kuwa ameridhika na utekelezaji wa mradi huo ambao unavutia na umekamiilika kwa asilimia 100.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.