Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Kenani Sawala ameridhishwa na zoezi zima la upigaji kura linavyoendelea katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura katika kituo cha 'Rest House' kilichopo Mtaa wa Shangani East, Kata ya Shangani, aliwataka Wananchi kuendelea kudumisha Amani na Utulivu mpaka zoezi hilo litakapokamilika.
"Nimefurahishwa na hali ya Wananchi kujitokeza kwa wingi wakiwa katika hali ya utulivu kama inavyoonekana hapa, na niombe wananchi wawndelee kuwa watulivu mpaka zoezi litakapokamilika," alisema Kanali Sawala.
Aidha aliwataka Wananchi wote waliojiandikisha kuhakikisha wanapiga kura kwani ni haki yao kidemokrasia na ndio Msingi wa kuwapata viongozi wanaowataka katika Mitaa yao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.