Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Kenani Sawala, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani na timu yake kwa usimamizi na matumizi mazuri ya pesa toka Serikali Kuu kukamilisha mradi wa Ujenzi shule ya Sekondari Tandika unaojengwa kwa fedha hizo.
Kanali Sawala ametoa pongezi hizo leo tarehe 18/11/ 2024 wakati wa ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi ndani ya mkoa wa Mtwara kwa kushirikiana na vyama vya siasa ili kujionea kazi nzuri inayofanywa na Raisi wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Amesema Ujenzi wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 560/- ni kielelezo tosha cha usimamizi kwa kasi na ubora wa fedha hizo kwani, fedha zilitolewa mwezi Juni, 2024, Ujenzi wake kuanza rasmi Agosti 2024 lakini hadi sasa ujenzi umeshafikia zaidi ya asilimia 90 ikiwa katika hatua ya umaliziaji.
"Kasi ni nzuri na tunaridhika na kasi hii na ubora unaoonekana..., hivyo kwa nafasi hii niwapongeze Mkuu wa Wilaya (DC) na MD (Mkurugenzi) na timu nzima, hongereni sana", amesema RC Sawala.
Sambamba na hilo amewapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kujitoa kwao katika ujenzi wa shule hiyo hali iiliyopelekea kupunguza gharama za Ujenzi, na akawataka wautunze ili mwakani uanze kupokea wanafunzi.
Vyama vya siasa vilivyoshiriki ziara hiyo ni pamoja na NCCR-MAGEUZI, CHADEMA, TLP, CUF, DP, UPDP, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, PPT Maendeleo, UMD, UDP, ADA-TADEA,
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.