Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Magdalena Rwebangira, amewataka Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Biometriki ngazi ya Kata kuwa makini wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu wapiga kura awamu ya pili ili kufikia malengo ya Taifa.
Rwebangira ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Biometriki ngazi ya Kata kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu wapiga kura awamu ya pili yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha STEMMUCO PARISH, leo tarehe 14 Mei, 2025.
Amesema umakini katika kazi hiyo itafanya kusiwe na makosa yatakayotia doa zoezi hilo.
Vilevile amewataka Wataalamu hao kuwa Mabalozi wazuri na mawakala kutoa taarifa sahihi kwa jamii ili washiriki kikamilifu zoezi hilo katika muda husika kwani hakutakua na muda mwingine baada ya zoezi hili kukamilika.
Aliongeza kuwa ni muhimu Kujiandaa kisaikolojia na kiutendaji, kuzingati muda wa kufunga na saa ya kufunga vituo sambamba na kuwepo vituoni hata kama wandikishwaji hawatakuwepo.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu wapiga kura awamu ya pili litaanza rasmi tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 22 Mei, 2025
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.