Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Magdalena Rwegasira ametembelea vituo vinavyotumika kwenye zoezi la uwekaji wazi na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili lililoanza Leo Mei 16 na linatarajia kumalizika Mei 25, 2025.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua vituo hivyo na kuona namna zoezi hivyo linavyoenda pamoja na kusikiliza changamoto na kuzipatia ufumbuzi
Zoezi la Uboreshaji wa Kudumu la Wapiga Kura linaenda sambamba na zoezi la uwekaji wazi wa daftari hilo ambapo wananchi wanapata fursa ya kukagua taarifa zao ili kama zimekosewa ziweze kurekebishwa kwenye zoezi la Uboreshaji.
Zoezi hilo linaenda na Kauli Mbiu Inayosema” Kujiandikisha Kuwa Mpiga ni Msingi wa Uchaguzi Bora.”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.