Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka viongozi ngazi ya Kata , halmashauri na wawezeshaji kushirikiana kwa Pamoja katika zoezi la ubainishaji na uandikishaji wa kaya mpya masikini zitakazonufaika na sehemu ya pili ya mpango wa TASAF awamu ya tatu ili kuwapata walengwa wanaostahili.
Ameyasema hayo April 19,2021 katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu kawaida alipofanya ufunguzi wa kikao kazi Cha kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa sehemu ya pili ya mpango huo.
Kyobya amesema kuwa katika kuiendea kazi hiyo wawezeshaji na viongozi wote watakaoshiriki katika zoezi hilo wanatakiwa kuwa waaminifu na waadilifu ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza hapo baadae.
Zoezi a Ubainishaji na Uandikishaji Litaanza rasmi April 26 mwaka huu likihusisha Mitaa 75 ya Kata 17 zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.