Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Ndugu Japhet Justine amesema kuwa Serikali imetoa shilingi Bilioni 401 kwa ajili ya kulipa madeni ya wakulima wa korosho wa Mkoa wa Mtwara kuanzia msimu wa 2018 hadi sasa.
Japhet amesema hayo Julai 22,2020 alipokutana na timu ya wataalamu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa ajili ya kutoa taarifa ya malipo ya madeni ya korosho na kujua fursa za uwekezaji zilizopo ambazo wao wanaweza kuwekeza.
Amesema kuwa hadi sasa tayari fedha zimeshaingizwa benki na kwamba kazi inayofanyika sasa ni kufanya uhakiki wa majina kwenye mfumo wa benki na kuhakiki akaunti za wakulima kama bado ziko hai (zinafanya kazi) ili hadi kufikia wiki ijayo kila mkulima awe ameshalipwa fedha zake.
Kuhusu kuwekeza katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani Japhet amemtaka mkurugenzi kuaandaa andiko la mradi linalohusu ujenzi wa soko la kisasa feri, ununuzi wa boti ya kuvulia samaki na ujenzi wa kiwanda cha Kusindika Samaki na kuliwasilishakatika Ofisi yake kw aajili ya Utekelezaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kulipa madeni ya wakulima wa korosho ya zaidi ya Milioni 844 katika Wilaya yake.
Aidha amemsiistiza Mkurugenzi na Timu yake kuchangamkia fursa waliyotioa TADB kwa kuandaa maandiko yenye tija na mazuri huku akiagiza Manispaa kuwapatia TIC, NACTE NA TADB maeneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ili kuwanufaisha wananchi wa Mtwara katika upatikanaji wa ajira na kuongeza mapato kwa halmashauri.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Juliana Manyama ametoa shukurani kwa benki ya Kilimo Tanzania kwa kuonesha nia ya kuwekeza katika Manispaa yetu kwani itaongeza thamani ya mazao katika maeneo yetu pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Aidha amewataka watu wengine kuja kuwekeza ndani ya Manispaa kwa kuwa yapo maeneo ambayo yameshatengwa kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo ujenzi wa viwanda mbalimbali na maghala ya kuhifadhia mazao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.