Serikali kununua ndege Sita hadi kufikia Julai 2018
Katika kuhakikisha kuwa Shirika la ndege Tanzania linaboresha huduma zake Serikali Imedhamiria kuiongezea mtaji shirika hilo ikiwa ni pamoja na na kununua ndege sita za kubeba abiria hadi kufikia Julai 2018.
Hata hivyo Serikali mpaka sasa imeshanunua ndege tatu aina ya bombardier ambazo zinafanya safari katika mikoa 10 ya Tanzania. Na kwamba hadi kufikia Julai 2017 ndege 3 zitakuwa zimeshanunuliwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandsi Edwin Amandusi Ngonyani katika sherehe za uzinduzi wa safari za ndege za ATCL “Bombadier Dash-8Q400” Mkoani Mtwara zilizofanyika mnamo tarehe 29 April 2017 katika viwanja cya kiwanja cha ndege Mkoani humo.
Mhandisi Ngonyani alisema kuwa dhamira ya serikali ya kununua ndege hizo itasaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja kutembelea vivutio vilivyopo Tanzania, Aidha aliongeza kuwa uwezo wa ndege hizo za kubeba abiria zinatofautiana kulingana na ukubwa ndege. Alifafanua kuwa ndege aina ya bombardier kila moja inaweza kubeba abiria 76, ndege 2 za masafa ya kati aina ya CS3 kila moja inauwezo wa kubeba abiria Na ndege kubwa ya masafa marefu aina ya boeing 7a78 itabeba abiria 262.
Aidha mhandisi aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma za anga kwa kukarabati Miundombinu ya viwanja vya ndege ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanja vipya ili viweze kutoa huduma bora.
Pia amewataka Wananchi wa Mtwara kutumia fursa ya usafiri kama huduma ya kawaida na itawapatia kipato
“Ninawomba wana mtwara tumieni fursa hii ya usafiri kama fursa ya kawaida lakini pia ni fursa ya kibiashara itakayowaongezea kipato cha mtu mmoja, familia na jamii.”alisema mhandisi Ngonyani.
Vilevile amewaaagiza wafanyakazi wa Shirikala ndege Tanzania kuwa waadilifu, wachapakazi, wenye kujituma , kuwa na maono na maarifa katika kutimiza azma ya Serikali ya Hapa kazi tu.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego ameishukuru Serikali kwa kuileta Bombadie na kwamba wana Mtwara wana imani kubwa na ndege hiyo akiamini kuwa uwepo w ATCL itawavutia wawekezaji kuja kuwekeza Mtwara na watalii kuja Mtwara.
Aidha Amemshukuru Rais kwa kutenga shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha uwanja wa ndege wa Mtwara na kwamba pesa hizo baada ya uboreshaji huo kutapandisha hadhi ya kuwa uwanja wa kimataifa. Aliendelea kusema kuwa fedha hizo zitajenga njia (run way), jengo la kisasa la kubeba abiria pamoja na ujenzi wa barabara ya kisasa ya kuingia kwenye uwanja.
Ndege za ATCL zitafanya safari yake Mtwara kwa wiki mara tatu ikiwemo siku ya Jumatatu saa 8.00 asubuhi, Jumatano saa7.00 mchana pamoja na Jumamosi saa 12 asubuhi, Aidha nauli kutoka Mtwara kwenda Dar ni sh.180,000/= na Mtwara-Ruvuma ni Tsh. 180,000/= kwa safari za kwenda , na kwa safari za kwenda na kurudi ni Tsh.180,000/=
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.