Serikali Wilayani Mtwara imekabidhi Shilingi laki tatu(300,000) ikiwa ni mkono wa pole kwa wanafunzi 35 wanaosoma Chuo Kikuu cha Stella Maris na Chuo Cha Utumishi wa Umma Mtwara ambao wameathiriwa na mvua kwenye hosteli wanayoishi ya Prorata iliyopo Kata ya Shangani katika Mtaa wa Kiyangu.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya amesema fedha iliyotolewa ni ya awali ambayo itawasaidia kununua chakula wakati Serikali ikiendelea kufanya jitihada zingine.
Aidha Mhe.Mwaipaya amewataka wanafunzi hao kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha nakuwasisitiza kusoma kwa bidii huku akiwataka kuwasiliana na viongozi pale wanapopata changamoto yoyote.
Nae Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Sixmund Lungu ametoa pole kwa wanafunzi hao kwa athari walizozipata huku akisema kuwa Manispaa itashirikiana na Wakala WA Barabara Mijini na Vijijini Wilaya ya Mtwara (TARURA) katika kuweka mikakati ya kuimarisha miundombinu ya barabara na mifereji ili kupunguza athari zitokanazo na mvua.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Emanuel Zengo, Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha SAUT Mtwara ameishukuru Serikali kwa msaada waliotoa kwa wanafunzi hao na ameiomba kuendelea kuwashika mkono kwa kuwa wanafunzi hao kwa sasa wana wanahitaji mengi kama vile chakula, madaftari ,taulo za kike na mahitaji mengine
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.