Serikali ya Tanzania imedhamiria kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kutoka Tani laki nne hadi Tani laki saba kufikia mwaka wa fedha wa 2025/2026.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Abbass Ahmed Abbass katika uzinduzi wa uhuishaji wa kanzi data ya wakulima wa zao la korosho uliofanyika katika Kata ya Naliendele mtaa wa Sogea Kwenye shamba la mmoja wa wakulima wakubwa wa zao hilo DR. Elly Kafiriti.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ili malengo hayo yaweze kutimia kila mdau anatakiwa kuweka mikakati thabiti katika eneo lake.
Ameitaja moja ya mikakati hiyo ni pamoja na uhuishaji wa kanzi data za wakulima ili Serikali iweze kuelekeza nguvu katika kuboresha huduma katika tasnia ya korosho inayosaidia kuongeza kipato cha mtu moja mmoja na Taifa.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa Rai kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa watakaofanya kazi ya uhuishaji wa kanzi data za wakulima kuifanya kazi hiyo kwa weledi na kutunza vifaa vyote vitakavyotumika .
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku ya pembejeo na kuendelea tafiti za mazao na mimea ili kuhakikisha eneo hili linafanya vizuri na lnaleta tija kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Brig.Jen.Mst Aloyce Mwanjile amesema kuwa uhuishaji huo utatumia mfumo wa kidijitali ulioandaliwa na Wizara ya Kilimo ambapo simu janja na visoma alama za vidole vitatumika katika zoezi hilo.
Mwanjile ameongeza kuwa uhusihaji huo ni sehemu ya maandalizi ya zoezi la usambazaji wa pebejeo za ruzuku liklaoanza April mwaka huu na amewataka wakulma kutoa ushirikiano kwa kujitokeza kuhuisha taariza zao wakiwa katika mashamba yao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.