Ili kuondoa udanganyifu uliokuwa unafanyika kwenye uombaji wa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na mamlaka za serikali za mitaa kupitia mapato yake ya ndani hapa nchini, Serikali imefanya mabadiliko ya utoaji wa mikopo hiyo kwa kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa mikopo ujulikanao kama Ten Percent loan management information system (TPLMISS)
Mfumo huo ulioanzishwa unawataka wanakikundi wanaotaka mikopo kuingia wenyewe kwenye mfumo na kujaza fomu za uombaji wa mikopo.
Hayo yamebainishwa Juni 30 ,2022 na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi .Juliana Manyama kwenye kikao kazi na wenyeviti wa serikali za Mitaa wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kilichofanyika katika Ukumbi wa Call nd Vision.
Manyama amesema kuwa mfumo huo ulioanzishwa hauondoi taratibu za awali za uombaji wa mikopo na kuwataka washiriki wa kikao kuhamasisha wananchi wao kujiandikisha NIDA ili waweze kupata vitambulisho vya Taifa kwa kuwa kwenye mfumo ulioanzishwa kipo kigezo cha uwepo wa Kitambulisho cha taifa kwa kila mtu anayeomba mkopo.
Kutokana na uwepo wa deni kubwa la mikopo ambalo Manispaa inadai kwa wananchi waliopewa mikopo na hawajarejesha, Manyama amewataka Wenyeviti wa Mitaa kusaidiana na Serikali katika kuwakumbusha wananchi waweze kurejesha fedha hizo ili wananchi wengine waweze kukopa.
Nae Mhagama Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa amewataka wenyeviti hao kujiepusha na rushwa kwnye zoezi zima la upitishaji wa fomu za maombi ya mkopo kwa watu wasio na sifa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.