Baada ya kumalizika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Tandika Mtwara na wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo kuanzia Januari mwaka huu, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu. Ismail Ali Ussi ameridhia kuzindua shule hiyo baada ya kukidhi vigezo vyote Leo Mei 25,2025.
Akizungumza wakati akiwa Shuleni hapo Ndugu. Ussi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi za kuimarisha sekta ya elimu hapa nchini hivyo wazazi wahakikishe wanawapeleka watoto shuleni wakapate elimu.
“Tumejionea maabara za kisasa, madarasa ya kisasa na maktaba za kisasa kwa kweli Rais ameleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya elimu,
“ Tumekagua shule yetu hii, ni nzuri, ina viwango, inapendeza, na imezingatia vigezo vyote vya kusoma watoto wetu amesema “ Ndugu Ussi
Shule ya Sekondari ya Tandika Mtwara imejengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa Sequip Shilingi milioni mia tano sitini mia tano ishirini na mbili mia nane ishirini na saba( 560,522,827) na fedha za michango ya wananchi Shilingi 2,050,000
Uwepo wa shule hiyo imesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shue za jirani na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea muda mrefu wa kwenda na kurudi shuleni .
Wazazi, wanafunzi na walimu shuleni hapo wametoa shukrani zao za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa shule hiyo kwani imesogeza huduma karibu na wananchi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.