Shule za Msingi na Sekondari ndani ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani zimefikia asilimia 94.4 ya utekelezaji wa mpango wa lishe - kwa utoaji chakula mashuleni kwa robo ya Julai hadi Septemba 2024.
Haya yamesemwa wakati wa kikao cha Tathimini ya Mkataba wa lishe ngazi ya kata, Robo ya kwanza Julai-Septemba 2024.
Kikao hicho kilichokua na lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe, kilihusisha jumla wa Watendaji Kata kutoka kata zote 18 pamoja na wataalamu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kiliongozwa na Tito Cholobi, Afisa Tarafa Mtwara Mjini akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa, Jumla ya idadi ya shule katika Halmashauri ni 56, ambapo shule msingi ni 36 na 24 za sekondari.
Idadi ya jumla ya Wanafunzi ni 28389 ambapo, idadi ya wanafunzi shule za msingi ni 18900 na Sekondari ni 9489.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.