Mkurugenzi wa Elimu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ephraim Simbeye amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya wasichana Mtwara yaliyogharimu Mil 160 hadi sasa.
Akizungumza katika ziara yake shuleni hapo Juni 7 mwaka huu Bw. Simbeye ametoa pongezi kwa wataalam na wasimamizi wa ujenzi huo kutoka Manispaa ya Mtwara -Mikindani kwa kuwa waaminifu katika umimamizi na utekelezaji wa majukumu yao na kuweza kubakiza fedha kutoka katika mradi mwingine wa ukarabati wa shule kongwe na kuwekeza fedha hizo katika ujenzi wa mabweni hayo mawili.
Ameendelea kuwasisitiza wataalam hao kuendelea kuwa waaminifu na wazalendo katika matumizi ya fedha ili kuipunguzia Serikali gharama zisizo na lazima.
"Niwapongeze mmeonesha uzalendo na uaminifu mkubwa sana, hii ndio inatakiwa tunatakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali kwa namna moja ama nyingine, maendeleo sio Serikali bali sisi wenyewe,endeleeni na moyo huo huo katika utendaji wenu”Alisema Simbeye
Ujenzi wa mabweni hayo yametokana na fedha zilizobaki katika ukarabati wa shule kongwe ambazo ni sekondari ya wasichana Mtwara na shule ya ufundi Mtwara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.