Diwani wa Kata ya Majengo Mhe.Sixmund Lungu ameibuka mshindi wa Uchaguzi wa Naibu Meya katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kwa asilimia 100 baada ya kupata kura 23 zilizopigwa na kuongoza kiti hicho Kwa mara ya pili mfululizo.
Mkuu wa divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bwana. George Mbogo amesema kuwa Halmashauri ilipokea jina Moja la Mgombea wa nafasi ya Naibu Meya kutoka Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi , hivyo Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi jina hilo limepigiwa kura za "Ndio" au "Hapana".
Akizungumza mara baada ya kutangazwa, Mhe.Lungu amewashukuru Madiwani Kwa kuendelea kumuamini na kumpigia kura zote za ndio kwani inaonesha namna Madiwani hao walivyo na imani kubwa na yeye na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuijenga Manispaa.
Uchaguzi huo umefanyika Leo Agosti 1,2024 Kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupitia na kujadili taarifa za halmashauri robo ya nne ya mwaka 2023/2024.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.