Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax amesema kuwa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu baina ya wananchi na Jeshi la wananchi Tanzania katika eneo la Mbae Mashariki unaenda kupata suluhu ndani ya mwezi wa tatu baada ya wizara yake kwenda kulishughulikia jambo hilo kwa mara nyingine tena.
Amesema kuwa suluhisho hilo litakuwa lenye manufaa kwa pande zote mbili kwa kuangalia usalama wa wananchi na usalama wa jeshi.
Mhe. Waziri ameyasema hayo Leo Machi 4, 2024 kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Mtaa wa Mbae Mashariki uliofanyika katika eneo la Pacha ya Kiolo.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa manufaa ya watu wote.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga amewataka wananchi kuheshimu mipaka ya Jeshi iliyowekwa na kuwaomba kutovamia maeneo hayo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.