Baada ya kufanya vizuri kwenye utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari ya mfano Kata ya Likombe na ujenzi wa jengo la kuhudumia wagojwa wa nje (OPD) , Maabara na Kichomea taka katika zahanati ya Ufukoni, Juni 11, 2022 tumetembelewa na ugeni kutoka halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Col.Patrick Sawala waliokuja kuona na kujifunza ni kwa namna gani tumetekelza miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora.
Halmashauri ya tandahimba ni ya pili kuja kutembelea miradi ikitanguliwa na halmashauri ya Mji Nanyamba
Manispaa ya Mtwara-Mikindani tumefurahi kupokea ugeni huo na tunaendelea kuwakaribisha wageni wengi Zaidi kuja kututembelea kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kuona mambo mengi mazuri yaliyopo kwenye Halmashauri yetu.
Mradi wa ujenzi wa Sekondari ya mfano Kata ya Likombe umegharimu shilingi milioni mia nne sabini (470,000,000) zilizotolewa na Serikali kuu huku ujenzi wa jengo la OPD, Maabara na kichomea taka katika Zahanati ya Ufukoni ukigharimu shilingi milioni mia mbili hamsini (250,000,000) kutoka kwenye fedha za tozo za miamala ya simu zilizotolewa na Serikali pia.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.