Serikali kupitia wakala wa barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Mtwara katika bajeti ya 2023/2024 imepanga kutumia Shilingi 2,690,380, 000 kwa ajili ya matengezo ya barabara zenye urefu wa km 160.63 makalavati 5 katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Meneja wa TARURA Wilaya ya Mtwara Ramadhani Mzingwa wakati akiwasilisha mpango wa bajeti ya matengenezo ya barabara 2023/2024 kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa kupitisha mpango na bajeti ya halmashauri uliofanyika Februari 3, 2023 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi
Mzingwa amesema kuwa fedha za ujenzi wa barabaraba hizo zinatoka kwenye vyanzo mbalimbali vikiwemo fedha za mfuko wa barabara (1,690, 380.000) ambazo zitafanya matengenezo ya barabara zenye urefu wa km 158.63 zikiwemo barabara km 124.77 za matengenezo ya kawaida, km 10.25 za matengenezo sehemu korofi , km 23.61 za matengenezo maalumu Pamoja na makalavati 5.
Kwenye fedha za Jimbo TARURA imepanga kutumia shilingi milioni mia tano (500,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Jamhuri yenye urefu wa km 0.5 na Jamhuri -Mangowela (km 0.5) kwa kiwango cha lami.
Aidha Kwenye fedha za Tozo shilingi milioni mia tano (500,000,000) zitaenda kujenga barabara ya Likonde – Mtawanya yenye urefu wa km 1 kwa kiwango cha lami..
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.