Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutokana na juhudi zake zilizofanyika katika kuboresha elimu kupitia mradi wa kuboresha elimu ya Sekondari (SEQUIP) na fedha kutoka Serikali Kuu huku ikiahidi kuendeleza ushirikiano na Manispaa hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Miradi na Utafiti Rasilimali, Masozi Nyirenda, alipofanya ziara katika Manispaa hiyo tarehe 08 Mei 2025, ili kuona maendeleo na miradi ya elimu.
Katika ziara yake Nyirenda alikuwa ameandamana na maafisa Masoko Bi.Janeth Mhegele na Prisca Msuya,amabo walishuhudiajinsi iradi hiyo ilivyotekelzwa kwa ufanisi.
Nyirend aameonesha kuridhdihswa na hatua zilizofikiwa akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-mMkindani ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa ajili ya Maendeleo ya elimu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa, Mwalimu Hassan Nyange ameishukuru TEA kwa ushirikiano mzuri wanaoupata na kuahidi kuendelea kusimamia kwa karibu miundombinu ili kuhakikisha kila mtoto anapata mazingira bora ya kujifunzia na kusomea,
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa mabweni Shule Ya Sekondari ya wasichana Mtwara, Ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi ya Rahaleo pamoja na ujenzi wa madarasa mawili Sekondari ya Likombe.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.