Timu ya Menejiment ya Halmashauri Manispaa Mtwara-Mikindani pamoja na waheshimiwa Madiwani wameshiriki kwenye zoezi la kumpokea Mkuu wa Mkoa mpya wa Mtwara Mhe. Glasius Gasper Byakanwa lililofanyika tarehe 30 Oktoba 2017 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo Mkuu wa Mkoa alizungumza na viongozi mbalimbali kwenye ukumbi wa Boma Mkoa huku akishukuru kwa mapokezi mazuri na kuomba ushirikiano kwenye suala zima la utendaji wa kazi.
Mkuu wa Mkoa huyo amesistiza Watendaji kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili tuweze kuwa salama.
Amesema anatambua kuwa mtu yeyote anayefanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu hapendwi hivyo amewataka watu wachape kazi kwani huwezi kuhangaika kumridhisha kila mtu.
Aidha amewaomba wana Mtwara kufanya mabadiiko makubwa kwenye Elimu ili tuweze kusimamia Rasilimali zetu vizuri
Pia ameahidi kukutana na Maafisa Elimu wote ili wamueleze sababu zilizopelekea Mkoa kufanya vibaya kwenye matokea ya Mtihani wa darasa la saba. Pamoja na hayo amewataka Wakuu wa Wilaya kutatua migogoro yote inayofika katika Ofisi zao ili kazi ya Mkuu wa Mkoa iwe Rahisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara Mohamedi Sinani amesema kuwa wao kama watafanya kazi bega kwa began a Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.