HAPA KAZI TU ni kauli ambayo Menejiment ya halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani inaitekeleza kwa vitendo kwa kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Hivi karibuni Serikali imetoa kiasi shilingi milioni 500 kwa baadhi ya halmashauri kwa ajili ya ukarabati wa majengo na ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwenye vituo vya afya iliyolenga kuboresha huduma za Mama na Mtoto
Fedha hizo zilitolewa na muongozo wa matumizi yake ikiwemo kuweka kipaumbele kwenye Ujenzi wa Jengo la upasuaji, Wodi ya mama na Watoto, Nyumba ya Mtumishi moja,Ujenzi wa Kichomea taka, Ujenzi wa sehemu ya kufulia nguo pamoja na Ujenzi wa Chumba cha kuhifadhi Maiti na Uimarishaji wa Mfumo wa Maji.
Manispaa Mtwara-Mikindani ni moja wapo ya halmashauri zilizopokea fedha hizo ambazo zimeelekezwa katika Ujenzi wa Wodi ya mama na Watoto, Nyumba ya Mtumishi moja, Ujenzi wa Maabara, Ujenzi wa sehemu ya kufulia nguo pamoja na Ujenzi wa Chumba cha kuhifadhi Maiti na Uimarishaji wa Mfumo wa Maji katika zahanati ya likombe.
Hadi kufikia tarehe 26 Oktoba 2017 Ujenzi wa Wodi ya Mama na watoto, Maabara na Sehemu ya kufulia nguo ukuta wa msingi umekamilika huku Chumba cha kulaza maiti zege kwa ajili ya ukuta wa msingi limeshamwagwa, na nyumba ya mtumishi setting ya msingi imeshaanza.
Timu ya Menejiment ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani ikiongozwa na Mkurugenzi Bi Beatrice Dominic walitembelea eneo la mradi kwa minajili ya kushiriki shughuli za Ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kushirikiana na mafundi ikiwa ni sehemu ya kuongeza hamasa ili mradi wote uwe umekamilika hadi kufikia Disemba 31 mwaka huu. Ili kufanikisha hilo menejimenti imepanga utaratibu wa kila siku ya Alhamisi katika wiki kuwa itashiriki Ujenzi wa miundombinu hiyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.