Timu ya Menejimenti ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani wakipatiwa mafunzo ya mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato (TAUSI) ambao umekuja kufanya maboresho ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa Serikali za mitaa (LGRCIS) unaotumika hadi sasa.
Bwana Zakaria Mkutano muwezeshaji wa mifumo kutoka TAMISEMI amesema kuwa mfumo huu unaanzishwa ili kuondoa changamaoto zilizokuwa zinajitokeza kwenye mfumo wa LGRCIS ikiwemo kuondoa orodha ya wadaiwa kwenye mfumo.
Amesema kuwa mfumo wa TAUSI utamuwezesha mtuamijai kutumia popote pale alipo na hivyo ukitumika vizuri utasaidia kuongeza mapato ya halmashuari.
Mafunzo ya mfumo wa TAUSI yamenza Julai 13 na yatamalizika Juni 17, 2022.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.