Timu ya Ukaguzi wa miradi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Januari 14,2023 imetembelea miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni mia tano sabini na nane (578,000,000)kutoka sekta ya afya na elimu na kuridhdishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo Pamoja na ubora wa majengo.
“Tumefanya ukaguzi wa miradi ili kujua imefikia wapi na ipo katika hatua gani,nilichokiona ni kuwa miradi yote ipo katika hatua nzuri, ubora wa majengo nimeridhika nayo, kiutendaji niseme mpo kwenye asilimia 95”amesema Patrick Kyaruzi Mkuu wa msafara wa Timu ya ukaguzi RS
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Dkt. Joseph Kisala maeishuru timu hiyo kwa pongezi walizotoa juu ya miradi iliyotekezwa na ameahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa .
Miradi iliyotembekewa ni Pamoja na ujenzi wa madarasa Matano Shule ya Sekondari ya Sino (100,000,000), ujenzi wa nyumba ya mtumishi Kituo cha afya Mikindani(60,000,000), Ujenzi wa nyumba ya mtumishi Zahanati ya Mtawanya (48,000,0000, Ujenzi wa madarasa matatu Shule ya Sekondari ya Shangani (60,000,000), ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi ya wazazi na jengo la kufulia Kituo cha afya Ufukoni (250,000,000) pamoja na Shule ya Sekondari ya Naliendele ujenzi wa nyumba vitatu vya madarasa (60,000,000).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.