Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wananufaika na uwepo wa gesi asilia katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) limetumia shilingi Milioni 30,052,500 Kujenga choo cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Shangani, Kukarabati vyoo na uchimbaji wa kisima cha maji katika shule ya Msingi ya Rahaleo zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Katifa fedha hizo shilingi Milioni18,600,000 zimetumika kujenga matundu ya vyoo shule ya Msingi Shangani na shilingi Milioni 14,452,500 zimetumika kukarabati matundu ya choo cha wasichana na uchimbaji wa kisima cha maji shule ya Msingi Rahaleo.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi miradi hiyo iliyofanyika Julai 16,2020, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Dunstan Kyobya amepongeza uongozi ya TPDC kwa kuguswa na kuamua kujitoa kujenga vyoo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na kwa wanafunzi wasichana wa shule hizo.
Pamoja na pongezi hizo pia Kyobya amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo waliopo Mtwara kuunga mkono jitihada za Serikali na kufuata nyayo za TPDC kwa kujitoa na kuchangia katika sekta ya elimu ili Wanafunzi wasome katika mazingira mazuri.
Aidha Kyobya ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye Watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) kuhakikisha kuwa Watoto hao hawakai nyumbani badala yake wapelekwe shuleni kwa ajili ya kupata Elimu kama Watoto wengine na kuwataka walimu kutoa taarifa katika vyombo husika endapo kuna mwanafnzi haudhurii masomo(utoro).
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi Juliana Manyama amewashukuru Shirika hilo kwa msaada walioutoa na kuwaomba kuendelea kusaidia katika shule zingine kwa kuwa mahitaji yako mengi.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini Bi. Marie Mselem amesema kuwa Shirika hilo limeweka utaratibu wa kurudisha kwa jamii kwa kuchangia katika sekta ya elimu, afya na utawala bora hivyo ujenzi wa choo bora kwa Watoto wenye mahitaji maalumu itawapelekea Watoto hao kusoma vizuri na kupenda kwenda shule.
Awali akisoma taarifa ya Shule Mwalimu MKuu wa Shule ya Msingi Shangani Bi. Marylce Elisha amesema kuwa jumla ya wanafunzi sabini na tano watanufaika na choo hiko na kuwashukuru Shirika hilo kuendelea kuchangia katika Shule kwa kuwa wanachangamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa madarasa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.