Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya @mwaipayaabdallah amepokea Mchele na Mafuta kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mtwara ikiwa ni msaada kwa waathirika wa mvua kubwa zilizonyesha Wilayani hapa.
TRA @tratanzania wamekabidhi msaada huo kupitia Kaimu Meneja TRA Mtwara, Daniel Katamboyi ambapo amekabidhi jumla ya kilo 250 za mchele pamoja na Mafuta ya kula Lita 90.
Mapema mwezi Februari Wilaya ya Mtwara ilianza kupata mvua nyingi na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo yake, hali iliyopelekea baadhi ya wakazi wake kupata changamoto ya kukosa chakula na uhalibifu wa miundombinu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.