TMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Mtwara imezindua wiki ya kutoa shukurani kwa mlipa kodi kwa kufanya usafi kwenye eneo la Stendi kuu ya zamani na soko kubwa lililopa Manispaa ya Mtwara-Mikindani lengo ikiwa ni kujenga mahusiano kati yao na wafanyabiashara ambao ndo walipa kodi.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mtwara EliRehema shayo amesema kuwa Pamoja na kujenga mahusiano TRA pia imelenga kuhamasisha wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwa Maendeleo ya Manispaa na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la Usafi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameipongeza TRA kwa kutambua thamani ya mlipa kodi kwa kufanya usafi kwenye maeneo yetu.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu kwa kufanya usafi kila wiki kwenye Kata ili kuuweka Mji wa Mtwara katika hali ya usafi pamoja na kuwaomba wanahabari kuendelea kuhamasiha juu ya wananchi kufanya usafi wa mazingira.
Ameendelea kumsisitiza Mkurugenzi kuweka vifaa vya kuhifadhia taka kwenye sehemu ambazo zina mikusanyiko ya watu wengi, kwenye barabara na sehemu mbalimbali ili mwananchi anapokuwa na uchafu aweze kuziweka humo badala ya kuzitupa hovyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko ameishukuru TRA kwa kujitolea kufanya usafi na amesema kuwa Manispaa ipo tayari kuwapokea wale wote wanaunga mkono Manispaa na amezikaribisha Taasisi nyingine wakipata nafasi wafanye kama ambavya TRA wamefanya.
Diwani wa Kata ya Chikongola Mussa Namtema amefurahishwa na zoezi la usafi Katika Kata yake na amesema kuwa wataendeleza utamaduni wa kufanya usafi Kila wiki yeye Pamoja na wananchi wake.
Wiki ya Kutoa shukurani Kwa Wateja imezinduliwa leo Novemba 19 na itamalizaka Novemba 24 mwaka huu .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.