Mstahiki Meya wa Manispaa Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile amewataka wananchi wote wa Manispaa kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kuepukana na magonjwa na kuimarisha afya.
Aidha Ndile amewapongeza wafanya biashara wa Soko la Samaki feri kwa kutunza mazingira katika eneo hilo na kuwasisitiza kuendelea na desturi ya kufanya usafi ili kuendeleza kuimarisha afya ya mlaji.
Pamoja na hayo Mstahiki Meya amewasisitiza wananchi hao kuchagua viongozi bora watakao waletea Maendeleo katika mitaa yao Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Rugembe Maiga amewashukuru wafanyabiashara wa soko hilo kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi na amewasisitiza kuendelea kuyatunza na kuyasimamia mazingira ili yaweze kuleta ustawi wa maisha endelevu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.