Ni Maeneo aliyoyasisitiza Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange Kwenye kikao Kiichowahusisha Viongozi wa vyama vya siasa vilivyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kwa ajili ya kupeana Miongozo na Kanuni na kuwaelekeza vituo vya Kupiga Kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
"Kuna watu wanatumia viongozi wa vyama kutugawa, Niwaombe tuingie Kwenye Uchaguzi tukiwa tumeshikamana na tuondoke tukiwa tukishikamana" amesema Mwalimu Nyange
Aidha amewaahidi kuwapa ushirikiano wa dhati wa kuijenga Mtwara.
Kwa upande wa Viongozi hao wamempongeza Msimamizi wa Uchaguzi Kwa kikao hiko ambacho kinaonesha muelekeo chanya kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa .
Viongozi waliohudhuria wanatoka Kwenye vyama vya siasa vifuatavyo CCM, CUF,ACT Wazalendo, DP,CHAUMA, SAUTI YA UMMA,NCCR-Mageuzi na CHADEMA
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.