Wakati nchi yetu ya Tanzania ikiadhimisha miaka 6o ya Uhuru , Leo Desemba 9 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.Jen.Marco Gaguti amewataka wananchi wa Mtwara kuienzi tunu na amani ya nchi yetu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na Usalama.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo Desemba 9,2021 kwenye maadhimisho ya maiak 60 yaUhuru yaliyofanyika Kimkoa eneo la Mji Mkongwe wa Mikindani uliopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hyo pia kuwataka wana Mtwara kujitoa sana katika kufanya kazi zenye tija ili kutoa mchango mkubwa kwenye kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi katika nchi yetu.
"Mchango wa Mkoa wa Mtwara katika pato la taifa kwa sasa ni asilimia 3 tuongeze juhudi katika shughuli za uzalishaji ili kiwango cha uchangiaji kifikie asilimia 5 na hili linawezekana .'amesema mhe. Gaguti
Ameendelea kusema kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa amejipanga kufanya kazi Mtwara kwa kuleta Maendeleo makubwa na kutaka wana Mtwara kumpa ushirikiano ili aweze kutimiza malengo yake.
Aidha amewashukuru wadau na wananchi wote walioshiriki katika kaundaa maadhimisho hayo yaliyofana.
Sherehe za maadhimisho ya Uhuru Kitaifa zinafanyika Katika Uwanja wa Uhuru uliopo Jijini Dar Es Salaaam na Mgeni rasmi ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasaan
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.