Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Francis Mkuti amewataka wauguzi kutumia changamoto zilizopo kuwa fursa ya kujiendeleza kielimu ili kuongeza kiwango cha mshahara na kuboresha mazingira mazuri ya ufanyaji kazi
Mkuti amezungumza hayo Mei 13,2018 kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ligula Mkuti na kuwasisitiza wauguzi wote wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kuwa na mahusiano mazuri kazini baina yao na madaktari wagonjwa ,wauguzi n ahata ndugu wa waggojwa
“Mkiwa na uhusiano mzuri basi mtafanya kazi kwa umoja kama timu ,na tujitahidi kuwaheshimu sana wagonjwa na ndugu zao maana ndio wateja wetu kazi zenu ni nyingi na chanagamoto ni nyingi tujitahidi sana kuwa na uhusiano mzuri na kila mmoja wetu”alisema Mkuti
Awali akisoma risalya ya wauguzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Veronika Kamwenda alisema kuwa wao kama wauguzi wamepata mafanikio makubwa tangu wameanza kutekeleza malengo ya milenia ikiwemo kutoa elimu ya afya kwa jamii juu ya uzuiaji wa magonjwa ya UKIMWI na kifua kikuu na malaria, kuwashirikisha akina baba kwa asiliimia 63 jatika huduma za afaya na uzazi pamoja na mafanikio mengine.
Siku ya Uuguzi Duniani inafanyika kila mwaka ifikapo tarehe 12 Mei na kitifa siku hii imeadhimishwa Mkoani ikiwa na kauli miu inasema “wauguzi ni sauti inayoongoza afya ni haki ya kila binadamu”.Manispaa imeadhimisha siku hii kwawauguzi Wauguzi kutoa vifaa vya kupimia joto wagonjwa (themometa) 15 kama zawadi kwa wagonjwa kupitia vituo vya afya ikiwemo Mtawanya(1), Ufukoni(1), Chuno(1), Naliendele(1) pamoja na Rwelu(1), zahanati ya Mikindani(3) na Likombe(3) pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa Ligula(4).
Pamoja na maadhimisho hayo wauguzi hao walikula kiapo cha utii mbele ya mgeni rasmi kama ahadi yao kuwa watafanya kazi zao kwa weledi na kwa kufuata kanuni,taratibu ,sera pamoja na miongozo iliyowekwa katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.