Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuendekea kuleta fedha Mkoani Mtwara kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoaa wa Mtwara Mhe. Yufus Nannila amewataka watumishi na viongozi Wilayani Mtwara kusimama na kumsemea mama Samia kwa wananchi mambo mazuri anayowatendea wana Mtwara.
Amesema kuwa ndani ya miezi tisa ya Uongozi wa Mama Samia ameleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya ambayo hadi sasa ameongeza vituo vya afya kumi na moja ndani ya Mkoa wa Mtwara.
Mhe.Nannila ameyasema hayo Januari 24,2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwenye kikao cha tathmini ya ziara yake kilichohusisha Viongozi wa Chama Pamoja na wataalamu kutoka halmashauri ya Nanyamba, halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Pamoja na Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Kutokana na Mkoa wa Mtwara kufanya vibaya kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha nne Mhe. Nannila ameziagiza Shule zote za Msingi na Sekondari Pamoja na Wilaya zote kuweka mikakati ya namna bora ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi.
“Ufulu Mkoani Mtwara ni mbovu, Chama Cha Mapinduzi hakijaridhika na matokeo ya kidato cha nne , viongozi tusaidiane ili kuona tatizo ni nini na tunachukua hatua za haraka , mwaka huu hatutaki daraja la nne wala sifuri” amesema mhe. Nannila
Aidha amezitaka shule zote kutambua mipaka yake huku akiziagiza halmashauri kuhakikisha maeneo yote ya shule na zahanati yanapimwa na kuandaliwa hati miliki ili kuondoa migogoro na wananchi lakini pia amezitaka shule hizo kuhakikisha zinaweka mfumo wa kuvuna maji ya mvua.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Thomas Salala amemshukuru mwenyeketi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara kwa kutembelea Wilaya ya Mtwara na kwamba maagizo na ushari uliotolewa na kamati hiyo utazingatiwa na kufanyiwa kazi ikiwemo kusimamia ufaulu shuleni Pamoja na kuwasimamaia wakurugenzi kutenga bajeti kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua kwenye shule, zahanati na Vituo vya afya.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.