TUNAMSHUKURU RAIS, WADAU KUTUSHIKA MKONO WANAMTWARA – RC SAWALA
Mkuu wa mkoa wa Mtwara COL. Patrick Sawala, amekabidhi rasmi vifaa vya maafa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya kwa ajili ya Kwenda kuvigawa kwa waathirika wa maafa ya mvua hizo kubwa zilizonyonyesha tarehe 3 – 7 Februari na kuleta madhara katika kata zote 18 za manispaa ya Mtwara – Mikindani.
Akizungumza katika halfa fupi ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya , leo Machi 13, 2025, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na wadau mbalimbali wajitolea kuchangia vifaa hivyo.
Alisema Rais Samia kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu ameipatia Mtwara vifaa na chakula cha kutosha ambavyo vikijumuishwa na vifaa vya wadau wengine vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafuta machozi waathirika wa maafa hayo.
Aidha, RC Sawala ametoa rai kwa wananchi wa Mtwara kuweka nyumba zao katika hali ya uimara ili kuzuia madhara kama hayo yasijitokeze tena.
Kwa upande wake DC Mwaipaya mbali na kuwashukuru wadau waliojitolea msaada mbalimbali, aliwashukuru pia wananchi waliojitoa kuwapa hifadhi wenzao waliopata maafa na akawata watendaji kusimamia vyema zoezi la ugawaji kwa wahusika.
Msaada uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Pamoja na wadau umejumuisha unga wa sembe, dona, mchele, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za unga, chumvi, sabuni za kuogea na taulo za kike.
Vingine ni magodoro, Blanketi, Vyandarua, nepi za kisasa(Diapers), Sahani, ndoo za lita 20 & 10, madumu Pamoja na mikeka.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.