Watoto wapatao elfu kumi na nane mia saba sabini (18770) kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani wanatarajia kupata chanjo ya polio katika Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo hiyo awamu ya tatu inayotarajia kuanzia tarehe 01/9/2022 na kumalizika tarehe 04/09/2022.
Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi.Sylivera Rugainisa amesema kuw achano hiyo inatolewa kwa watoto wote waliowahi kupata chanjo na wasiopata chanjo wenye umri chini ya miaka mitano.
Amesema kuwa watoa huduma wa chanjo watapita kila mtaa kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kuaznia saa 1. 00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.
Aidha Bi. Rugainisa ametoa wito kwa wazazi na walezi wote kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata chanjo ya polio ili kuwakinga na ulemavu wa viungo na kukoa maisha ya watoto hao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.